Isaiah 49:20-25


20 aWatoto waliozaliwa wakati wa msiba wako
bado watakuambia,
‘Mahali hapa ni finyu sana kwetu,
tupe eneo kubwa zaidi la kuishi.’

21 bNdipo utasema moyoni mwako,
‘Ni nani aliyenizalia hawa?
Nilikuwa nimefiwa, tena tasa;
nilikuwa nimehamishwa na kukataliwa.
Ni nani aliyewalea hawa?
Niliachwa peke yangu,
lakini hawa wametoka wapi?’ ”

22 cHili ndilo asemalo Bwana Mwenyezi: “Tazama, nitawaashiria watu wa Mataifa,
nitainua bendera yangu kwa mataifa;
watawaleta wana wako mikononi yao,
na kuwabeba binti zenu juu ya mabega yao.

23 Wafalme watakuwa baba zenu wa kuwalea,
na malkia wao watakuwa mama zenu wa kuwalea.
Watasujudu mbele yako nyuso zao zikigusa ardhi;
wataramba mavumbi yaliyo miguuni mwako.
Ndipo utajua ya kuwa Mimi ndimi Bwana;
wale wanaonitumaini mimi hawataaibika.”


24 dJe, nyara zaweza kuchukuliwa kutoka kwa mashujaa wa vita,
au mateka kuokolewa kutoka kwa watu wakali?

25 eLakini hili ndilo asemalo Bwana: “Naam, mateka watachukuliwa kutoka kwa mashujaa,
na nyara zitapokonywa kutoka kwa watu wakali.
Nitashindana na wale wanaoshindana nawe,
nami nitawaokoa watoto wako.
Copyright information for SwhKC